YAS yaja na EXTRA MILE

kwa kutambua umuhimu wa uhakika, uthabiti na msaada wa haraka kwenye miamala ya simu wanahakikisha wanaenda extra mile katika kuwahudumia wateja wao.

YAS yaja na EXTRA MILE

Wateja wa Yas na Mixx wataweza kupata msaada wa huduma moja kwa moja masokoni kote nchini, huku wakijishindia zawadi katika maduka ya kampuni hizo, kupitia Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyozinduliwa leo jijini Mwanza na itakayoendelea hadi Oktoba 9.


Uzinduzi huo umefanyika Rock City Mall,jijini Mwanza ambapo viongozi mbalimbali wa chapa hizo wamesema kaulimbiu ya mwaka huu, 'The Extra Mile', inasisitiza wajibu wa kwenda hatua ya ziada katika kumhudumia mteja, ikiwemo kumsikiliza, kumpa msaada kwa wakati na kutimiza ahadi anazopewa.

Advertisement EATV


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mixx, Arnold Ngarashi, amesema kwa kutambua umuhimu wa uhakika, uthabiti na msaada wa haraka kwenye miamala ya simu wanahakikisha wanaenda extra mile katika kuwahudumia wateja wao.



Katika wiki hii, maduka ya Yas na Mixx yatakuwa na shughuli za kusherehekea pamoja na wateja, ambapo wateja watajishindia zawadi mbalimbali kupitia michezo shirikishi kama kuzungusha gurudumu na kujibu maswali.

Moja kati ya maduka ya huduma kwa wateja ya YAS
Moja kati ya maduka ya huduma kwa wateja ya YAS


Moja ya maduka ya YAS

You can share this post!

TULIA AKEMEA UNYANYASAJI DHIDI YA WANAWAKE

UKATILI WA WATOTO

Related Posts