WATOTO 175 WALAWITIWA,KUBAKWA NA KUTELEKEZWA WANGING'OMBE 2025/26 SERIKALI YAKUCHUKUA HATUA KALI
WATOTO 175 WALAWITIWA,KUBAKWA NA KUTELEKEZWA WANGING'OMBE 2025/26 SERIKALI YAKUCHUKUA HATUA KALI
Licha ya adhabu kali na elimu zinazotolewa kila uchwao ,katika Halmashauri ya wilaya ya Wangin'ombe Mkoani Njombe Bado inakabiliwa na tatizo kubwa la ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto ambapo takribani matukio 175 ya kubakwa,kulawitiwa,kutelekezwa na ukatili wa kimwili yameripotiwa huku wanao tajwa kuhusika na ukatili huo wakiwa ni ndugu na wafanyakazi wa familia hususani wanochunga mifugo kama ng'ombe na mbuzi.
EMMANUEL MKULU NA TAARIFA ZAIDI........................
Wakieleza ukubwa wa tatizo la ukatili wa kijinsia hususani kwa watoto,visababishi na hatua zinazopaswa kuchukuliwa maofisa ustawi na maendeleo ya jamii wilaya ya Wanging'ombe akiwemo Yohana Sewando wamesema hali ni mbaya na inatakiwa kupigwa vita na jamii nzima ili kuokoa watoto wetu na hata wazee hususani wanaume kwakuwa wanatengwa na watoto wao na kuwasababishia sonona.
Cue in Yohana Sewando -Msoma Taarifa ya Ustawi Wanging'ombe
Cue in Plasida Ndeluka-afisa Ustawi Wanging'ombe
Cue in Rehema Muhunzi-Afisa Ustawi Wanging'ombe
Kukithiri kwa matukio haya kumenilazimu kuongea na makundi tofauti katika jamii za wilaya hiyo wakiwemo wanafunzi ambapo wanasema shida kubwa na tamaa ya mali na kimwili hivyo hatua zaidi zichukuliwe dhidi ya waarifu.
Cue in Ernest Lihabusia mkazi wa Mngate
Cue in Sarah Mwagike Mkazi wa Mdandu
Cue in Morine Marua Mwanafunzi Wanike Sekondari
Awali akikazia suala la ukatili dhidi ya watoto na wazee mgeni rasmi ambae pia ni katibu tawala wilaya ya Wanging'ombe Veronica Gerard amesema kila mtu anajukumu la kulinda watoto na kukemea kitendo cha watoto kutoa kipaumbele kwa mama pekee wakati wa uzee.
Cue in Veronica Gerard -Katibu Tawala(DAS)Wanging'ombe