TULIA AKEMEA UNYANYASAJI DHIDI YA WANAWAKE

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dkt. Tulia Ackson, amekemea unyanyasaji dhidi ya wanawake, akisisitiza kuwa vitendo hivyo katika uongozi na siasa vinakiuka haki za binadamu na misingi ya demokrasia. Akizungumza katika Mkutano wa Wabunge Wanawake wa IPU jijini Arusha, Dkt. Tulia amesema Tanzania imeweka mikakati ya kupinga unyanyasaji huo, huku Spika wa Bunge Mussa Zungu akisema wanawake wanachangia kwa asilimia 39.5 ya uwakilishi ndani ya Bunge.

TULIA AKEMEA UNYANYASAJI DHIDI YA WANAWAKE

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dkt. Tulia Ackson, amekemea unyanyasaji dhidi ya wanawake katika sekta mbalimbali, ikiwemo uongozi na siasa.


TAARIFA ZAIDI NA JOHN LUPOKELA....

Advertisement EATV


Dkt. Tulia ameyasema hayo leo, Oktoba 5, 2026, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wabunge Wanawake wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Arusha (AICC).


Amesema wakati wa uongozi wake waliunda sera na kuweka mikakati ya kupinga unyanyasaji dhidi ya wanawake, akisisitiza kuwa unyanyasaji katika uongozi na siasa haukubaliki kwa kuwa unakiuka haki za binadamu na misingi ya demokrasia.


Dkt. Tulia amesema msimamo wake wa kupinga unyanyasaji huo hautabadilika, huku akisisitiza umuhimu wa jamii kujenga utamaduni wa kuzingatia usawa wa kijinsia ili wanawake wawe salama na waishi kwa amani.


Naye Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Zungu, amesema utawala bora ni ule unaoweka kipaumbele katika ushiriki wa wanawake kwenye masuala ya uongozi na siasa, pamoja na kuimarisha demokrasia.


Ameeleza kuwa Tanzania imepiga hatua katika kuleta usawa wa kijinsia, akisema Bunge la Tanzania linawakilishwa na wanawake kwa asilimia 39.5.


Mkutano huo uliofanyika leo ni sehemu ya mikutano inayofanyika katika Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), unaofanyika nchini Tanzania.

MWISHO

You can share this post!

YAS yaja na EXTRA MILE

Related Posts