Jumla ya wagonjwa 42 waliozaliwa na tatizo la mdomo wazi wamefanyiwa upasuaji katika kambi maalum ya matibabu iliyofanyika mkoani Iringa, kwa lengo la kurekebisha tatizo hilo na kuwawezesha kurejesha uwezo wa kula, kuzungumza na kuendelea na shughuli zao za kila siku.
Jumla ya wagonjwa 42 waliozaliwa na tatizo la mdomo wazi wamefanyiwa upasuaji katika kambi maalum ya matibabu iliyofanyika mkoani Iringa, kwa lengo la kurekebisha tatizo hilo na kuwawezesha kurejesha uwezo wa kula, kuzungumza na kuendelea na shughuli zao za kila siku.
Tatizo la mdomo wazi ni hali ya kuzaliwa ambayo inaweza kumuathiri mtoto katika ulaji wa chakula na uwezo wa kuzungumza, sambamba na changamoto za kijamii na kisaikolojia.
Kupitia kambi hiyo iliyoendeshwa kwa ushirikiano na shirika la Operation Smile, wagonjwa waliotimiza vigezo wamepatiwa huduma ya upasuaji bila malipo."Wagonjwa walipimwa, na wale waliokuwa wanafaa kufanyiwa upasuaji ndio wamefanyiwa..."DKT ALFRED MWAKALEBELA, mganga mfawidhi hospitali ya rufaa iringa
Kwa baadhi ya familia, huduma hiyo imekuwa zaidi ya matibabu, kwani imewapa watoto waliokuwa wakiishi na tatizo hilo tangu kuzaliwa nafasi ya kuanza maisha mapya wakiwa na matumaini."Yaani mpaka watu wanaulizana, maana huduma hii tulidhani haiwezekani..."MWASHABANI mohammed, mkazi wa kilwa"Kwakweli watu wenye changamoto za watoto wenye mdomo wazi waje, maana inawezekana."HAWA SALUM, mkazi wa mtwara
Pamoja na huduma hiyo kuendelea kutolewa, bado kuna haja ya kuongeza uelewa wa jamii kuhusu tatizo la mdomo wazi, ikiwemo uwepo wa huduma za matibabu na uwezekano wa kufanyiwa upasuaji."Kwakweli jamii bado muamko ni mdogo, ila tunaendelea na elimu..."DKT RADHIA BAKARI, mratibu wa huduma za wagonjwa, operation smile"Sisi kwakweli tunawashukuru sana, maana ilikuwa kama ndoto..."– JOSEPH MTENGA, mkazi wa iringa
Kambi hiyo ni sehemu ya juhudi za kuwafikishia wananchi huduma za matibabu, hususan wale wanaohitaji huduma maalum za upasuaji ambazo wakati mwingine hazipatikani kwa urahisi katika maeneo yao.