ALIYETOWEKA NA MTOTO WA MIEZI 10 AKAMATWA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kumpata mfanyakazi wa ndani, Angel Abayo, mwenye umri wa miaka 19, aliyedaiwa kuondoka na mtoto mwenye umri wa miezi 10 kutoka eneo la Kibada, Kigamboni.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Faustine Mafwele, amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa Abayo aliondoka na mtoto huyo kwa lengo la kwenda kumsalimia dada yake aliyekuwa amepata ajali eneo la Kibaha.

Advertisement EATV

Mafwele amesema uamuzi huo ulifuatia baada ya mwajiri wake kumkatalia ruhusa ya kwenda kumwona ndugu yake huyo aliyekuwa amejeruhiwa katika ajali.

Amesema Jeshi la Polisi lilianza kufuatilia tukio hilo mara baada ya kuripotiwa na, kwa kushirikiana na wananchi pamoja na wadau wa ufuatiliaji, lilifanikiwa kumpata mtoto huyo pamoja na Abayo ndani ya muda mfupi.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewashukuru wananchi na wadau wengine kwa ushirikiano wao uliowezesha kupatikana kwa mtoto huyo kwa haraka.

You can share this post!

wagonjwa 43 wafanyiwa upasuaji mdomo wazi

Related Posts