KITAIFA 02
Kiungo mshambuliaji wa Dodoma Jiji, Berno Ngassa, amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Septemba wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/27, huku Fikiri Elias wa Coastal Union akichaguliwa Kocha Bora. Ngassa aliwashinda Maabad Maabad wa Coastal Union na Anuary Jabir wa Polisi Tanzania.
Ngassa alitoa mchango mkubwa katika michezo miwili ya timu yake iliyoshinda yote, akifunga bao moja na kuhusika katika jingine. Kwa upande wa Fikiri, aliyeingia fainali na Steve Barker wa Simba na Vincent Mashami wa Dodoma Jiji, aliiongoza Coastal Union kushinda michezo yote miwili na kupanda kutoka nafasi ya 15 hadi ya 11 katika msimamo wa ligi.
Wakati huo huo, Ligi Kuu inatarajiwa kurejea kesho, Oktoba 7, kwa michezo mitatu. Mashujaa itacheza na Polisi Tanzania saa 8:00 mchana, Pamba Jiji dhidi ya Geita Gold saa 10:15 jioni, huku Namungo ikimenyana na TRS United saa 12:30 jioni.
NGASSA MCHEZAJI BORA SEPTEMBA
Fikiri Elias Kocha bora Septemba
Ngassa aisaidia Dodoma Jiji kushinda
Coastal Union yapanda nafasi nne
Ligi Kuu kurejea kesho Oktoba 7
BERNO NGASSA WA DODOMA JIJI NA KOCHA FIKIRI ELIAS WA COASTAL UNION WATWAA TUZO MWEZI SEPTEMBA WA LIGI KUU