Mchezaji wa tenisi wa Marekani, Coco Gauff WEB
Mchezaji wa tenisi wa Marekani, Coco Gauff

MZOZO WA COCO GAUFF  CHINA

COCO GAUFF, AKUMBWA NA TUHUMA ZA ‘UDANGANYIFU’ LICHA KUTINGA 16 BORA CHINA OPEN

KIMATAIFA 02

Mchezaji wa tenisi wa Marekani, Coco Gauff, amekumbwa na mzozo wa tuhuma za ‘udanganyifu’ baada ya kusimamisha mchezo katikati ya rally alipokuwa akipoteza pointi dhidi ya Mchina mwenye umri wa miaka 16, Sun Xinran, katika China Open. Gauff alikuwa nyuma kwa 5-4 katika seti ya kwanza baada ya kupiga mpira vibaya, kabla ya Sun kurejesha mpira na kushinda pointi hiyo, lakini Gauff akasimama na kuinua mikono akidai kulikuwa na mwanga uliokuwa ukimulika kwa kusuasua pembeni mwa uwanja.


Advertisement EATV

Baada ya tukio hilo, pointi hiyo ilirudiwa na Gauff akabadilisha kabisa mchezo, akishinda michezo yote iliyofuata isipokuwa mmoja na kumchapa Sun na kutinga hatua ya 16 bora jijini Beijing. Baadaye Gauff alitumia mtandao wa X kueleza kuwa alisimamisha mchezo baada ya kuona mwanga huo ukimulika tena, akisisitiza kuwa kanuni zinaruhusu mchezaji kupinga au kuomba marudio ya pointi kutokana na changamoto kama hiyo.


Gauff pia alikanusha vikali tuhuma za udanganyifu na kukumbwa na mashambulizi ya kibaguzi kwenye mitandao ya kijamii, akisema amepokea jumbe nyingi za kibaguzi baada ya tukio hilo. Aidha, alisema alimwomba radhi Sun Xinran baada ya mchezo na mchezaji huyo kuelewa hali iliyotokea. Gauff sasa anakwenda kukutana na Mbelgiji Elise Mertens katika hatua ya 16 bora ya China Open.


MZOZO WA COCO GAUFF  CHINA

Gauff asimamisha rally dhidi Sun

Gauff atuhumiwa kufanya udanganyifu China

Gauff akanusha tuhuma za udanganyifu

Gauff ataja mashambulizi ya kibaguzi

COCO GAUFF, AKUMBWA NA TUHUMA ZA ‘UDANGANYIFU’ LICHA KUTINGA 16 BORA CHINA OPEN

You can share this post!

NGASSA MCHEZAJI BORA SEPTEMBA

F1 YATAKIWA KUJITATHMINI