RONALDO AGOMA KUSTAAFU

RONALDO AGOMA KUSTAAFU

CRISTIANO RONALDO AMESEMA HANA MPANGO WA KUSTAAFU KUICHEZEA TIMU YA TAIFA YA URENO

KIMATAIFA 01

Cristiano Ronaldo amesema hana mpango wa kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Ureno na yupo tayari kurejea baada ya kumaliza adhabu yake ya kusimamishwa. Ronaldo amesema Rais wa Shirikisho la Soka la Ureno (FPF) alimshawishi kuendelea na timu hiyo, huku akieleza kuwa kocha wa sasa ndiye anayefaa kuiongoza Ureno.


Advertisement EATV

Ronaldo amesema kocha huyo alimweleza kuwa ni sehemu muhimu ya mipango yake na angeanza katika mchezo wa kwanza na wa mwisho, huku akipendekeza asafiri kwenye baadhi ya michezo ya ugenini. Hata hivyo, Ronaldo alikataa pendekezo hilo akisema kama nahodha hawezi kubaki nyumbani. Katika mchezo dhidi ya Norway, alikubali kucheza dakika 30, lakini hakutumiwa licha ya kuanza kupasha misuli kipindi cha pili.


Nyota huyo ameomba radhi kwa wachezaji wenzake kwa kuondoka kambini na mashabiki kwa kutowasalimia baada ya mchezo. Amesema yuko tayari FPF kumchukulia hatua bila kupunguziwa adhabu, akisisitiza kuwa jukumu hilo ni lake kama nahodha. Ronaldo ameongeza kuwa licha ya mazungumzo ya kuandaliwa mchezo wa kumuaga, bado anataka kuendelea kushindana na Ureno.


RONALDO AGOMA KUSTAAFU

Ronaldo kuendelea kuitumikia Ureno

Nyota huyo akubali adhabu ya FPF

Ronaldo aomba radhi kwa kuondoka kambini

Mshambuliaji huyo ataka kuendelea kushindana

CRISTIANO RONALDO AMESEMA HANA MPANGO WA KUSTAAFU KUICHEZEA TIMU YA TAIFA YA URENO

You can share this post!

F1 YATAKIWA KUJITATHMINI

MKATABA MPYA ARTETA HADI 2030