Joseph
namenamenamename

CHANGAMOTO YA MICHE YA KAHAWA MBINGA DC KUPATIWA UFUMBUZI HALMASHAURI YATOA TANI I ZA MBEGU.

Kwa kiasi kikubwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga wanajishughulisha na kilimo cha kahawa, ambacho kimeinua sana uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na halmashauri kwa ujumla. Hata hivyo, wananchi hao wanakumbwa na changamoto ya upatikanaji wa miche ya zao hilo. Katika kutatua changamoto hiyo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, amekabidhi tani moja ya mbegu za kahawa kwa vyama vya msingi vya ushirika 20 vya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mbegu bora za kahawa kwa vyama vya msingi vya ushirika 20 vilivyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga tarehe 7/10/2026, Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, amesema kwa kiasi kikubwa wananchi wa Wilaya ya Mbinga wanaendesha uchumi wao kupitia zao la kahawa. Amesema kuwa katika kuondoa changamoto ya upatikanaji wa miche ya kahawa, halmashauri imetoa tani moja ya mbegu kwa lengo la kuzalisha miche milioni 3.5, ambayo itaongeza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na halmashauri kwa ujumla.

Advertisement EATV

Zao la kahawa kwa sasa limeinua kwa kiwango kikubwa uchumi wa vijana wa Mbinga, ambapo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma, Oddo Mwisho, amewataka vijana kuacha tabia ya kukimbilia mijini kupiga debe. Aidha, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, Desiderius Haule, amewaagiza viongozi wa AMCOS za Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga waliopata mbegu za kahawa kusimamia vizuri uzalishaji wa miche katika maeneo yao ili kumaliza changamoto ya upatikanaji wa miche.

Kwa upande wao, viongozi wa AMCOS waliokabidhiwa mbegu za kahawa wamesema changamoto ya upatikanaji wa miche ya kahawa ni kubwa sana, hivyo hatua zilizochukuliwa na halmashauri za kukabidhi mbegu kwa wananchi zitasaidia kutatua changamoto hiyo.

You can share this post!